Home news BAADA YA VIKAO VIIINGI…HATIMAYE CHAMA HUYU HAPA..WAMOROCO WAKUBALI YAISHE….

BAADA YA VIKAO VIIINGI…HATIMAYE CHAMA HUYU HAPA..WAMOROCO WAKUBALI YAISHE….


Inaelezwa kuwa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia, Clatous Chotta Chama amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu ya RS Berkane ya Morocco.

Chama alisajiliwa na RS Berkane kwa mkataba wa miaka mitatu mwanzoni mwa msimu huu, akitokeza kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC.

Taarifa zinaeleza kuwa Mkataba wa Chama na RS Berkane utakoma rasmi Januari 2022, na atakua huru kujiunga na klabu yoyote ndani na nje ya Afrika, huku Simba SC ikipewa kipaumbele cha kumsajili.

Sababu kubwa ya Chama kusitisha mkataba wake klabuni hapo ni kushindwa kukabiliana na hali ya hewa na chakula nchini humo.

Wakati Chama akifanya maamuzi ya kuvunja mkataba wake, Usajili wa Dirisha Dogo kwa Tanzania linafunguliwa rasmi kesho Jumatano (Desemba 15).

SOMA NA HII  RASMI...MBEYA KWANZA YAWA YA KWANZA KUSHUKA LIGI KUU MSIMU HUU...GEITA GOLD WAISOGELEA CAF KININJA...