Home news UWANJA MPYA SIMBA ‘MAMBO NI MOTO’…UONGOZI WATOA TAMKO…WACHEZAJI WAHUSISHWA….

UWANJA MPYA SIMBA ‘MAMBO NI MOTO’…UONGOZI WATOA TAMKO…WACHEZAJI WAHUSISHWA….


MAMBO ni moto. Ujumbe aliouposti Rais wa Heshima wa Simba, bilionea Mohammed ‘Mo’ Dewji kwamba atatoa Sh2 bilioni kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa uwanja wao mkubwa kwa ajili ya kuchezea mechi kule Bunju, watendaji wameanza kwenda mbio kuhakikisha jambo hilo linatimia.

Mo kupitia ukurasa wake wa (Instagram), jana aliandika: “Wanasimba wenzangu wameshauri tujenge uwanja wetu na wako tayari kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo. Naomba kuweka wazi kwamba nimepokea maoni hayo kwa mikono miwili,” Mo Dewji aliandika.

“Naomba bodi ya Simba kukaa na kuja na utaratibu wa haraka ili jambo hili lianze utekelezaji, kwa kuanza naahidi kuchangia Sh2 bilioni, nawaomba Wanasimba wote tuchangie.”

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi Simba, Mulamu Nghambi alisema mpango huo ni habari njema kwa mashabiki wa Simba na wapenda maendeleo ya soka la nchi hii na kwamba mchakato huo tayari umeanza haraka.

“Huu mpango ulianza zaidi ya miaka miwili nyuma. Wachezaji wetu, benchi la ufundi chini ya Pablo Franco kabla ya mchezo na Red Arrows ule wa hapa nyumbani walitembelewa na viongozi na kati ya mambo waliyoambiwa ni kuanza mchakato huu wa ujenzi wa uwanja wetu wa nyumbani,” alisema Mulamu na kuongeza;

“Tuliwambia wale wachezaji watakaokuwa kwenye kikosi misimu mingine mbele watashuhudia hili na watakuwa kwenye historia ndani ya timu kucheza mechi kwenye uwanja wetu wa nyumbani.”

Ramani ya Simba ni ile ambayo uwanja wao utabeba mashabiki 30,000 na ni wazi watahitaji vyanzo zaidi vya kukamilisha ujenzi huo. Uwanja wa Benjamini Mkapa unaobeba mashabiki 60,000 uligharimu dola milioni 56 (sawa na zaidi ya Sh.112 bilioni).

SOMA NA HII  KISA 'KAGOLI KAMOJA' JANA....GAMONDI AOMBA RADHI YANGA...