Home Habari za michezo KISA ‘KAGOLI KAMOJA’ JANA….GAMONDI AOMBA RADHI YANGA…

KISA ‘KAGOLI KAMOJA’ JANA….GAMONDI AOMBA RADHI YANGA…

Habari za Yanga SC

Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo FC, jana Jumatano, Septemba 20, 2023 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam.

Bao pekee la Yanga lililofungwa na Mudathir Yahya katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC dakika ya 88, baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukuwa nafasi ya Pacome Zouzoua na kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo wakifikisha pointi tisa.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema kuwa ilikuwa kazi ngumu kucheza na namungo kwa sababu ni kama walikuwa wameususia mpira na kuwaacha Yanga wacheze kisha wao wakabe njia zao.

“Nadhani wote mmeuona mchezo, tulijaribu kutengeneza nafasi ili kupata ushindi, upande mwingine walikuwa wakipoteza muda na refa aliwaangalia tu. Hatukucheza vizuri, lakini tumefunga bao moja na kupata ushindi.

“Ukicheza na timu ambayo haitaki kucheza siku zote itakuwa ngumu, tungeshinda kipindi cha kwanza huenda tungepata mabao mengi zaidi, Max alipata nafasi lakini hatukufunga.

“Ninaomba radhi kwa hilo kwa sababu pia hata wao walikuwa wakitushambulia na wametengeneza nafasi nyingi tu. Hata mechi zilizopita ambazo tulishinda bao tano kila mechi hazikuwa mechi nyepesi, zilikuwa ngumu.

“Leo (jana) hatukuwa wazuri kwenye kupiga pasi, tumepoteza nafasi nyepesi, hatukuwa bora lakini hili ni soka, nimepata alama tatu na nimeshasahau,” amesema Gamondi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUISHIA JUKWAANI MSIMU ULIOPITA...MAKAMBO AVUNJA UKIMYA KUHUSU YANGA MPYA...ATOA MSIMAMO WAKE...