Home Simba SC JOHN BOCCO AKABIDHIWA MKWANJA WAKE LEO

JOHN BOCCO AKABIDHIWA MKWANJA WAKE LEO


 BAADA ya Mei 22 nahodha wa Simba John Bocco kuteuliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo, leo Mei 24 amekabidhiwa zawadi yake aliyoahidiwa.

Bocco amekabidhiwa zawadi ya Tsh. 2,500,000, (Milioni 2 na nusu) baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs.

Zawadi hiyo imetolewa na kampuni ya Emirate
Aluminium Profile.


Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Simba ilishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Kaizer Chiefs ambapo Bocco alitupia mabao mawili.
Licha ya ushindi huo Simba ilikwama kutinga hatua ya nusu fainali kwa sababu mchezo ule wa awali uliochezwa nchini Afrika Kusini, ubao ulisoma Kaizer Chiefs 4-0 Simba.
Hivyo wawakilishi wa Tanzania, Simba wametolewa hatua ya robo fainali kwa aggregate ya Simba 3-4 Kaizer Chiefs.
SOMA NA HII  MABEKI HAWA WAWILI SIMBA WAZAWA NI WAZEE WA KAZI,DAKIKA KIBAO