Home Habari za michezo A-Z JINSI SIMBA SC WALIVYOIBAMBA WYDAD KWA MKAPA….ISHU NZIMA ILIANZAI HAPA…

A-Z JINSI SIMBA SC WALIVYOIBAMBA WYDAD KWA MKAPA….ISHU NZIMA ILIANZAI HAPA…

Habari za Simba SC

DAKIKA 90 za mchezo wa mkondo wakwanza kati ya Sinba SC na Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Wydad Casablanca umemalizika kwa Simba kupata ushindi wa bao 1-0.

Simba SC ambayo itatakiwa kusafiri kwa ajili ya mchezo wa marudiano kule Morocco Aprili 29 itakuwa na kazi ya ziada ya kulinda bao hilo ili kusonga kwenye hatua ya nusu fainali.

Simba SC ilijipatia bao lao pekee kwenye mchezo huu kupitia straika wao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean Baleke dakika ya 31.

Baada ya bao hilo Simba ilionekana kulisakama zaidi lango la Wydad ambapo Kibu Dennis na Sadio Kanoute walipiga mashuti kadhaa langoni kwa Wydad lakini hayakuzaa matunda.

Kipindi chapili pili Simba ilionekana kutawala zaidi mchezo lakini hakuna shambulizi lao lililozaa matunda hadi filimbi ya mwisho inapulizwa.

Baada ya mchezo huu Wydad imefunga jumla ya mabao 14 katika michuano hii kiujumla na kati ya mabao hayo imefunga matatu tu katika viwanja vya ugenini ikianza kufanya hivyo dhidi ya Rivers United kwenye raundi ya kwanza ya kufuzu hatua ya makundi, pia ikaenda kufunga mabao mawili kwenye mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Petro de Luanda.

Morocco ndio nchi iliyoingiza timu nyingi(2), kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa msimu huu ambazo ni Wydad na Raja Casablanca.

Simba pia katika michuano hii hadi sasa imefunga mabao 18 ambayo sita ilifunga ikiwa ugenini na yaliyobakia imefunga ikiwa uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  SIMBA KWA MISIMU MIWILI SASA WAMESHINDWA NA WATANI ZAO