Home Uncategorized MTIBWA SUGAR:TUTAFANYA VIZURI 2020/21

MTIBWA SUGAR:TUTAFANYA VIZURI 2020/21


 THOBIAS Kifaru, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar amesema kwa sasa wanaamini watafanya vizuri licha ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zubeir Katwila kubwaga manyanga na kuibukia Klabu ya Ihefu.


Kwa sasa Mtibwa Sugar ipo chini ya Vincent Barnaba ambaye ni kocha msaidizi ndani ya Mtibwa Sugar na mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi alishinda bao 1-0 dhidi ya Namungo FC.


Akizungumza na Saleh Jembe, Thobias Kifaru amesema kuwa timu yao ipo imara na itafanya vizuri ndani ya ligi licha ya kuwa Katwila ameondoka.


“Ni kweli Katwila ameondoka lakini hakuna namna kwa kuwa alikuwa ni kijana wetu na tumekaa naye kwa muda mrefu, hamna shida kwa sasa maisha lazima yaendelee.


“Tupo vizuri na kila mchezaji anajua kwamba ndani ya Mtibwa Sugar kila mchezaji anafurahia na wakati uliopita tuliumia kwa nini timu inakosa matokeo ilihali kila kitu kipo sawa.

“Kwa sasa tunazidi kujiweka sawa na imani yetu ni kwamba mechi zijazo tutafanya vizuri mashabiki watupe sapoti katika hili,” amesema.

  

SOMA NA HII  YANGA YAIFUATA KAGERA SUGAR NA MATUMAINI YA KUTOSHA