Home Uncategorized KIONGOZI SIMBA ALIPATA TABU SANA NA BAO LA MORRISON ALILITAZAMA KWENYE WHATSAPP

KIONGOZI SIMBA ALIPATA TABU SANA NA BAO LA MORRISON ALILITAZAMA KWENYE WHATSAPP

OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amefunguka kuwa bao ambalo walifungwa na Yanga kwenye mechi ya Dabi ya Kariakoo Machi 8, aliliangalia kwenye Makundi ya WhatsApp baada ya kushindwa kutazama mechi hiyo.
Manara amesema kwamba bao hilo alishindwa kulitazama kwa sababu alizima simu zake ambazo zilikuwa na uwezo wa kutazama mechi hiyo. Wakati wa mechi hiyo Manara alikuwa nchini Hispania.
Bao hilo lilifungwa na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison na kuifanya Yanga kushinda kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
 Manara amesema kwamba mechi nzima kati ya timu hizo aliifuatilia kwa kupitia komenti za makundi ya WhatsApp baada ya kuzima simu ambayo alikuwa akiiangalia mechi hiyo mwanzoni tu mwa mechi kabla ya kufungwa.

“Baada ya mechi kuanza nilizima simu ambayo nilikuwa ninaangalia mechi, nikabaki na simu ambayo watu walikuwa wanachati kwenye magroup, nilipoona kelele zinazidi nikajua tumefungwa na baadaye nikamini tutarudisha haikuwa hivyo,” amesema.
SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA