Home Uncategorized GSM NA YANGA SASA WAJA NA STAILI MPYA YA USAJILI

GSM NA YANGA SASA WAJA NA STAILI MPYA YA USAJILI

WADHAMINI wa Yanga, Kampuni ya GSM wamerejea kivingine klabuni hapo na safari hii wamekuja na staili mpya ya usajili kwa wachezaji wa kimataifa ambayo ili usajiliwe ni lazima uichezee timu ya taifa ya nchi yako.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu GSM watangaze kurejea kuendelee na udhamini wa nje ya mkataba ikiwemo posho, mishahara wa wachezaji na benchi la ufundi, kambi za wachezaji na usajili ambayo ilifanikisha usajili wa Bernard Morrison, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Yikpe Gnaimen.
GSM imerejea Yanga ni baada ya hivi karibuni kutangaza kujiondoa kwenye udhamini wa timu hiyo kufuatia baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji kudai wadhamini hao wanaingilia majukumu ya viongozi likiwemo suala la usajili.
Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kwa sasa wataendelea kufanya ushirikiano na GSM kwa kuwa ni wanafamilia na wanaipenda timu ya Yanga.

“GSM ni wanafamilia wa Yanga wanaipenda timu ndio maana wapo nasi bega kwa bega, wamekuwa nasi kwenye nyakati mbalimbali na wamefanya makubwa ikiwa ni pamoja na kutupa sapoti wakati wa kambi pale Tanga tulipocheza na Coastal Union hivyo bado kuna tupo nao pamoja,” amesema.
SOMA NA HII  BREAKING: BOCCO ATEULIWA KUWA NAHODHA WA TIMU YA TAIFA