Home Uncategorized DE BRUYNE WA MANCHESTER CITY HATIHATI KUKOSA MANCHESTER UNITED

DE BRUYNE WA MANCHESTER CITY HATIHATI KUKOSA MANCHESTER UNITED

PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Manchester City ametoa tamko ambalo linaonyesha dalili kuwa kuna uwezekano mdogo wa nyota wake Kevin De Bruyne kuanza mechi ya kesho dhidi ya Manchester United.

City itamenyana na United kesho kwenye mchezo wa Ligi Kuu England utakaopigwa Uwanja wa Old Trafford ambao utakuwa ni wa kukata na shoka.

Guardiola amesema kuwa nyota wake huyo hayupo sawa kutokana na kusumbuliwa na maumivu.

“Kevin De Bruyne ana maumivu makali kwa sasa aliyapata baada ya kuanguka kwenye mchezo wetu dhidi ya Aston Villa bado sijajua mambo yatakuaje tunafuatilia hali yake,” amesema.

SOMA NA HII  VIDEO: YATAZAME MABAO MANNE YA MCHEZO KATI YA TANZANIA PRISONS V AZAM FC