Home Uncategorized BEKI WA JUVENTUS RUGANI: SIKUWA NA DALILI ZA CORONA

BEKI WA JUVENTUS RUGANI: SIKUWA NA DALILI ZA CORONA


DANIELE Rugani, beki wa Juventus amesema kuwa hakuwa na dalili zozote za Virusi vya Corona licha ya vipimo kuonyesha kuwa ana Virusi hivyo.

Beki huyo wa Kati alionekana na Virusi hivyo ambavyo vinasambaa kwa kasi duniani na kusababisha mechi za Ligi Kuu Italia (Serie A) kusimamishwa kwa muda bado anasisitiza kuwa yupo fiti.

Nyota huyo mwenye miaka 25 amesema kuwa kupata Virusi hivyo kutamsaidia kuongeza ufahamu wake kuhusu Virusi hivyo.


 “Nipo fiti na nimekua poa sana sijawahi pata dalili za Corona ambazo mnazisoma kwenye habari. 

“Nilikuwa na bahati licha ya kupata Virusi hivyo nilikuwa wa Kwanza kuvipata kwenye mazingira yangu na matumaini yangu itaongeza ufahamu wangu,” .

SOMA NA HII  SIMBA YAMFUATA MKALI ZAIDI YA MORRISON, MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI