Home Uncategorized SVEN: WACHEZAJI WAPO VIZURI, BADO TUNAENDELEA KUWAREJESHA KWENYE UBORA

SVEN: WACHEZAJI WAPO VIZURI, BADO TUNAENDELEA KUWAREJESHA KWENYE UBORA


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa wanaendelea kuwarejesha wachezaji wao kwenye utimamu wa mwili kabla ya kuanza kuwafanyisha mazoezi magumu.

Simba ambao ni mabingwa watetezi walianza mazoezi tangu Mei 27 kwenye Uwanja wao uliopo Bunju kwa ajili ya kujiandaa na mechi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa anaamini kwa kadri siku zinavyozidi kwenda wanarejea kwenye ubora wao.

“Taratibu wachezaji wanarejea kwenye ubora wao kwani hatukuwa nao pamoja kwa muda mrefu hivyo ni lazima tuanze kuwarejesha katika hali yao taratibu.

“Kwa program ambazo wanazifanya ni rahisi kwao kurejea katika ubora wao ambao walikuwa nao awali kabla ya ligi kusimamishwa,” amesema.

SOMA NA HII  MAMA WA BEKI WA YANGA KUZIKWA LEO