Home Uncategorized MTIBWA SUGAR YAACHANA NA ISHU YA GHARAMA WALIZOTUMIA TANGA

MTIBWA SUGAR YAACHANA NA ISHU YA GHARAMA WALIZOTUMIA TANGA


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa umeachana na suala la kufikiria gharama walizotumia kujiaandaa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union na badala yake wanarejea Morogoro kuvunja kambi.
Kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa na Serikali kutokana na kusambaa virusi vya Corona, Machi 17 Mtibwa Sugar ilitakiwa icheze na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani jana Machi 18.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa walikuwa wamemaliza maandalizi yote kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union kabla ya mchezo huo kusitishwa kwani Corona ni jambo la dunia.
“Tulikuwa na mchezo dhidi ya Coastal Union kila kitu kilikuwa sawa tulishawasili tayari na kila kitu kilikuwa sawa ilikuwa tunasubiri muda tu wa kumalizana na Coastal Union, kwa sasa tunarejea Morogoro ili kuendelea na masuala mengine huku tukiomba suala hili lipite salama,” amesema Kifaru.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa imecheza mechi 29, imeshinda mechi nane na imeambulia sare tisa kama ilivyo kwa Mbeya City ambayo yenyewe ipo nafasi ya 17 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
SOMA NA HII  PAMBA SC WAISHUKURU TPLB NA TFF KWA MKWANJA WA MILIONI MOJA, WAJA NA OMBI JINGINE