Home Uncategorized WACHEZAJI YANGA WACHELEWESHA KUANZA KWA KAMBI

WACHEZAJI YANGA WACHELEWESHA KUANZA KWA KAMBI

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa wa kuweka kambi upo mikononi mwa wachezaji wa kigeni na ndani hivyo wakifika wote wataanza kambi.

Akizungumza na Saleh Jembe, mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa mpango mkubwa ni kwa timu kuanza kambi mapema ila kinachowachelewesha ni wachezaji wa kigeni pamoja na wa ndani ambao bado hawajasawasili.

“Tayari kwa sasa wachezaji wameanza kuwasili Bongo, hivyo wakishafika wote tutakaa chini na kupanga wapi tutakwenda kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao,” amesema.

Wachezaji ambao wametia timu Bongo kwa ajili ya maadalizi ya msimu ujao ni pamoja na Issa Bigirimana, Juma Balinya na Kalego.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YATUMA UJUMBE HUU KWA KMC