Home Uncategorized KOCHA SIMBA ATAJA KINACHOMFELISHA IBRAHIM AJIBU

KOCHA SIMBA ATAJA KINACHOMFELISHA IBRAHIM AJIBU

KOCHA wa zamani wa kikosi cha Simba na Dodoma FC, Jamhuri Khiwelu ‘Julio’ amesema kuwa nyota mpya wa Simba, Ibrahim Ajbu ana uwezo na kipaji kikubwa kuliko nahodha wa timu ya Taifa, Mbwana Samatta anayekipiga KRC,Genk.

Julio amesema kuwa kinachombeba Samatta ni juhudi na kujituma hivyo kama Ajibu atafanya hivyo atakuwa mbali.

“Huwa ninamwambia mara kwa mara Ajibu kila ninapokutana naye kwamba ana kipaji kikubwa zaidi ya Samatta hivyo anapaswa afuate nyayo za nyota huyo anayekipiga Genk.

“Kama ataongeza juhudi na nidhamu atafikia malengo yake kwa wakati kuliko ilivyo sasa kwani bado muda wa mafanikio upo kwake,” amesema.

SOMA NA HII  SARPONG ACHEKELEA KUIBUKIA YANGA, ATOA AHADI HII