Home Uncategorized SIMBA KAZI BADO IPO LEO TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED

SIMBA KAZI BADO IPO LEO TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED


KIKOSI cha Simba kilicho chini ya Mbelgiji, Sven Vandenbroeck kimecheza jumla ya mechi 27 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Kimeshinda mechi 22 ambazo ni nyingi kuliko timu nyingine zilizocheza mechi 27.

Mbinu ya sare kwake ni ngumu kwani kina sare mbili ambazo ni Sawa na dakika 180.

Kupokea kichapo kimeonja ladha ya kupoteza mechi tatu ambazo ni Sawa na dakika 270 na kuyeyusha jumla pointi tisa.

Kwa upande wa mabao ya kufunga kina hazina ya mabao 55 ambayo pia ni mengi kuliko timu zote zilizocheza mechi 27.

Kimetunguliwa mabao 15 ndani ya Ligi Kwa mechi zake ilizocheza na kibindoni ina pointi 68.

Ipo nafasi ya Kwanza kwenye Msimamo na Leo itamenyana na Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa Uwanja wa Uhuru majira ya saa 10:00 Jion

SOMA NA HII  WAPINZANI WA YANGA WAINGIWA NA MCHCHETO MKUBWA