Home Uncategorized WAPINZANI WA YANGA WAINGIWA NA MCHCHETO MKUBWA

WAPINZANI WA YANGA WAINGIWA NA MCHCHETO MKUBWA


Shoo ya Yanga na Township Rollers kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika itapigwa jijini hapa Jumamosi saa 10:30 jioni lakini jamaa wameanza kuingiwa mchecheto.

Kwanza wamepunguza viingilio huku wakipigia magoti mashabiki wajazane kwa wingi kama Yanga walivyowafanyia Taifa kwenye sare ya bao 1-1. Kiingilio cha chini Jumamosi ni 2000 na cha juu 10,000.

Winga wa Rollers Motsholetsi Sikele ambaye ndiye mashabiki wanamtegemea awavushe, amewapa
angalizo kwamba Yanga hii si ile ya kipindi kile na kwamba sapoti yao inahitajika kwa kiasi kikubwa kwa vile kazi bado ni ngumu.

Sikele amesema kuwa wanapata hofu ya kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo kutokana na ubora wa kikosi cha Yanga ambacho wamekuwa wakikifuatilia na kugundua kwamba kinazidi kubadilika. “Yanga si wale wakati ule, ni timu imara na yenye malengo.

“Tunawaomba mashabiki wa Rollers wote kwa pamoja kujitokeza kwa wingi katika mchezo wetu
kama wale wa Yanga walivyojaa kwenye mechi ya kwanza.

“Tunahitaji sapoti yao itakayotuwezesha sisi kupata matokeo mazuri katika mchezo huu wa nyumbani, Yanga siyo nyepesi kama ilivyokuwa ya msimu uliopita ambayo tulikutana nayo mwaka 2018. Hii ya sasa ipo fiti na ina uwezo wa kupiga pasi hadi 20, hivyo tuna kibarua kigumu kuelekea mchezo huu,”alisema mchezaji huyo.

Wiki iliyopita kipa wao namba moja alidokeza kwamba anahofia sana guu la kushoto la Patrick Sibomana na analifanyia kazi ya ziada mazoezini

SOMA NA HII  ISHU YA KUFUNGIWA MASHABIKI JKT TANZANIA WAOMBA MSAMAHA