Home Uncategorized BANDA AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUMTAKIA KHERI YA KUZALIWA

BANDA AWASHUKURU WATANZANIA KWA KUMTAKIA KHERI YA KUZALIWA

ABDI Banda beki wa timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga kwenye Klabu ya Highlands Parks amewashukuru watazania wote ambao wamemtakia kheri kwenye siku yake ya kuzaliwa.

Banda amesherehekea sherehe yake ya kutimiza miaka kadhaa akiwa ndani kutokana na kutoruhusiwa kutoka ndani kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Banda amesema:”Nawashukuru watanzania wote ambao wamenitumia ujumbe na kunikatika kila la kheri kwenye siku yangu ya kuzaliwa na wale ambao ninaishi nao huku Afrika Kusini.

“Kwa sasa ninachukua fursa ya kusema asante ila nimeshindwa kusherehekea na wenzangu kutokana na kutoruhusiwa kutoka nje kwani tunashinda ndani kwa sasa,” .

SOMA NA HII  EDEN HAZARD APATA KIGUGUMIZI KUTOFAUTISHA PREMIER LEAGUE NA LA LIGA