Home Uncategorized DILI LA NYOTA ANAYEWINDWA NA YANGA PAMOJA NA SIMBA LAINGIA DOA, HAWA...

DILI LA NYOTA ANAYEWINDWA NA YANGA PAMOJA NA SIMBA LAINGIA DOA, HAWA HAPA WAMETIBUA


HASSAN Zidadu, Mwenyekiti wa Klabu ya Namungo amesema kuwa mkataba wa nyota wao Relliants Lusajo unameguka hivi karibuni ila wameanza mazungumzo naye.

Lusajo ambaye ni nahodha wa Namungo FC amekuwa kwenye ubora wake msimu huu ambapo ametupia mabao 11 na pasi tatu za mabao.

Inaelezwa kwa tayari mabosi wa Yanga na Simba walianza kumpigia hesabu nyota huyo hivyo kwa hatua ambayo mabosi wake wameanza nayo huenda wakaambulia patupu.

Zidadu amesema:”Tunatambua mchango wake ndani ya kikosi chetu ila kikubwa ambacho tumeanza kukifanya kwa sasa ni mazungumzo naye kuona namna gani ataongeza mkataba ndani ya kikosi chetu.

“Amekuwa kwenye ubora wake na anatimiza majukumu yake vizuri, tupo naye kwenye mazungumzo mambo yakikamilika ataendelea kuitumikia klabu yetu,”.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU PENALTI MBILI ZA KAGERE