Home Habari za michezo HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU MSIMU HUU 23/24…..SIMBA VS YANGA MAPEMAAA...

HII HAPA RATIBA YA LIGI KUU MSIMU HUU 23/24…..SIMBA VS YANGA MAPEMAAA TUU…

Yanga SC na Simba SC

RATIBA ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2023/24 inatarajia kuanza Agosti 15 mwaka huu hadi Mei 29, 2024, ambayo imetoka jana huku pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, itachezwa katika raundi ya nane ambayo itakuwa Novemba 8, mwaka huu.

Mchezo huo ambao Simba atakuwa mwenyeji unaenda kuwa na taswira ya kipekee baada ya timu hizo kufanya usajili mzuri utakaopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam saa 11:00 jioni.

Mechi mbili kubwa zingine ni kati ya Yanga dhidi ya Azam FC utakaopigwa Oktoba 25 saa 12:00 jioni .

Simba dhidi ya Azam FC watakutana Novemba 28, mwaka huu, saa 11 : 00 jioni mechi zote mbili kuchezwa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Pazia la ligi hiyo linatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti 15 mwaka huu huku mzunguko wa kwanza zitakutanisha timu sita kwa michezo mitatu ikiwemo Ihefu FC dhidi ya Geita Gold FC utakaopigwa katika Uwanja wa Highland Estate, uliopo Mbarali, utachezwa saa 10:00 Alasiri.

Michezo mingine ni kati ya Namungo FC ikiwakaribisha JKT Tanzania katika dimba la Majaliwa, uliopo Ruangwa, Dodoma jiji FC dhidi ya Coastal Union, Agosti 16, Mashujaa watawakaribisha Kagera Sugar katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

Agosti 17 kutakuwa na michezo miwili kati ya Azam FC dhidi ya Kitayosce FC mchezo utakaochezwa uwanja wa Azam Complex , uliopo Chamazi, Mtibwa Sugar dhidi ya Simba Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Singida Fountain Gate FC itawakaribisha Tanzania Prisons katika dimba la Liti Singida utakaochezwa Agosti 22 na 23 mwaka huu Yanga dhidi ya KMC FC katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, Almas Kasongo alisema ratiba wamezingatia ratiba za mashindano yote ya kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za Taifa.

Alisema walifanya kazi kubwa sana kupanga ratiba hiyo kwa kuepuka viporo vingi kwa kuzingatia michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa klabu mbili za Simba na Yanga pamoja na kombe la Shirikisho Afrika ambazo Azam FC na Singida Fountain Gate FC.

“Tumeangalia pia mashindano ya kombe la Mapinduzi ambayo Tanzania Bara kutoa timu tano zinaenda visiwani kwenda kwenye mashindabo hayo , Kombe la Shirikisho la FA, Michuano ya AFCON 2023 ambapo Tanzania tutacheza September mwaka huu, CHAN 2024 zinazotarajia kufanyika Guinea inashiriki kutakuwa na raundi tatu, awali, ya pili na tatu zote zitakuwa nyumbani na ugenini

Michuano mingine ya AFCON ya 2025 na kombe la Dunia mwaka 2026 zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico pia ratiba imeangalia mashindano hayo,” alisema Kisongo.

Aliongeza kuwa wamefanya mazungumzo ma wanaosimamia mashindano ya Super League na kutaka kuwaondoa timu ya Simba katika kipindi cha Oktoba 20 hadi Novemba 21, mwaka huu kwa sababu ya kumpa nafasi ya kujiandaa na michuano hiyo.

“Baada ya kukutana na waaandaji hao walitueleza kuwa ratiba ya michuano hiyo bado haijatoka na kutarajia kutoka kati ya wiki ya pili ya September wametusisitizia kuwaondoa Simba katika tarehe hizo kwa kuwapa nafasi ya kufanya maandalizi mazuri.

“Tunatambua mashindano hayo yanayoshirikisha timu nane kubwa barani Afrika na Tanzania ni wenyeji ya mashindano hayo huku Simba ikiwakilisha Taifa letu, hali hiyo tumeamua kupanga ratiba kuwa rafiki kwa kuzipa nafasi wawakilishi wetu katika michuano ya kimataifa kufanya vizuri,” alisema Kasongo.

Kuna shindano la Super League ambalo Simba inashiriki kuanza Oktoba 20 hadi Novemba 21 Tanzania kuwa wenyeji na droo itatangazwa kati kati ya wiki ya pili Septemba .

“Tumekutana na mazingira magumu ya kupanga ratiba kwa sababu ya mashindano mengi yaliyopo hapa nchini ikiwemo kwa timu zetu nne zinaenda kushiriki,” alisema Kassongo.

SOMA NA HII  HAJI MWINYI.: YANGA SC BADO HAIJAPATA BEKI KAMA MIMI....WALINIFANYA NIKAPOTEZA 'DEMU'...

5 COMMENTS