Home Uncategorized SINGIDA UNITED INA KIBARUA KIGUMU LEO MBELE YA SIMBA IKIWA IPO NAFASI...

SINGIDA UNITED INA KIBARUA KIGUMU LEO MBELE YA SIMBA IKIWA IPO NAFASI YA 20


SINGIDA United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ramadhan Nswanzurimo imecheza jumla ya mechi 27 kwenye Ligi Kuu Bara.

Imeshinda mechi mbili na kujivunia pointi sita katika mechi hizo ilizocheza ndani ya msimu wa 2019/20.

Imepoteza mechi 19 ikiwa ni idadi kubwa ya mechi za kupoteza kwa timu moja ndani ya Ligi kwa msimu huu.

Imelazimisha Sare mechi sita na kufanya isepe na pointi sita kwenye mechi hizo mbili.

Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 14 idadi ambayo ni ndogo kuliko timu zote zilizocheza mechi 27 msimu huu.

Kwa upande wa mabao ya kufungwa imeruhusu jumla ya mabao 40 mzigo mkubwa wa mabao kuliko timu zote na ina pointi 12 kibindoni zinazoifanya iwe nafasi ya 20.

Leo itakuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na Simba.

SOMA NA HII  MKENYA ANAYEKIPIGA NDANI YA SIMBA QUEENS ATAJA SABABU ZA KUCHEZA SOKA