Home Azam FC KOCHA MSOMALI WA AZAM AKUBALI YAISHE KWA YANGA…KAONA ISIWE TABU…KAAMUA AJE NA...

KOCHA MSOMALI WA AZAM AKUBALI YAISHE KWA YANGA…KAONA ISIWE TABU…KAAMUA AJE NA HILI…


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Azam Abdi Hamid Moallin amesifia ubora wa kikosi cha Yanga na kujipanga kuandaa mbinu ili kuwakabili vijana hao wa Jangwani ambao wapo kwenye kiwango kizuri kwa sasa nchini.

Akiongea na waandishi wa habari Afisa Habari wa Klabu ya Azam Zaka Zakazi amesema:

“Baada ya kocha wetu kufahamu kuwa katika mchezo unaofuata tutacheza dhidi ya Yanga alipata nafasi pia ya kupitia takwimu zao kwa ujumla na ameniambia Yanga ndiyo timu bora zaidi katika Ligi yetu kwa sasa hivyo sisi tunaenda kupambana nao kama underdog.”

Klabu ya Yanga na Azam zinakutana kesho katika pambano la Ligi Kuu Bara maarufu kama Ligi Kuu ya NBC katika Uwanja wa Chamanzi Dar es Salaam ambapo Azam atakuwa mwenyeji wa mchezo huo.

SOMA NA HII  MBABE WA YANGA CAFCC AJIUZULU