Home Uncategorized SIMBA YAWAPIGIA HESABU NYOTA HAWA WANNE, SVEN ATAJA SABABU

SIMBA YAWAPIGIA HESABU NYOTA HAWA WANNE, SVEN ATAJA SABABU

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anahitaji nyota wapya wanne ndani ya kikosi chake ambao wataongeza nguvu msimu ujao.

Sven ambaye ameiongoza Simba kwenye mechi 18 amesema anahitaji washambuliaji wawili na viungo wawili.
“Tuna kikosi kizuri hapa na nafikiria tutaendelea na kila mmoja aliyepo japokuwa tutahitaji wachezaji kadhaa wapya katika kila nafasi, kuna maeneo ya kuongeza watu kwenye kikosi hiki cha sasa,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwindwa na Simba ni pamoja na Lukas Kikoti wa Namungo na Baraka Majogoro wa Polisi Tanzania ambao ni viungo huku kwa upande wa washambuliaji ni Lusajo Reliants wa Namungo na Paul Nonga wa Lipuli.
  
  
SOMA NA HII  BREAKING: SARRI AFUNGASHIWA VIRAGO JUVENTUS