Home Habari za michezo JULIO;- SIMBA NIPENI KAZI MFURAHI…YANGA WANAFANIKIWA KWA SABABU YA WATU KAMA SISI…

JULIO;- SIMBA NIPENI KAZI MFURAHI…YANGA WANAFANIKIWA KWA SABABU YA WATU KAMA SISI…

Habari za Michezo

Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameutaka uongozi wa Simba kuwaamini wachezaji wao wa zamani akiwemo yeye ili kuipa timu hiyo maendeleo.

Julio alisema, kwa uwezo wake na nguvu aliyoitoa akiwa Simba, anastahili kuwa hata mshauri wa benchi la ufundi ili kuinyanyua timu hiyo.

Julio alisema: “Wenzetu Yanga, wanafanikiwa sana, mtu kama Said Maulid, mdogo wangu Mtwa (Mwanamtwa Kihwelo) wapo pale, timu kubwa ikiwa inacheza wanakwenda uwanjani na wanatoa mchango wao.

“Simba nipeni kazi hapo niwaoneshe, mimi nafanya kazi ya ushauri wa benchi la ufundi la Taifa Stars, mimi ni kocha wa timu za vijana, nitashindwaje kuwasaidia Simba?” alihoji Julio.

SOMA NA HII  YANGA WAAMUA KUISHUSHIA KMC MAMBO YA TP MAZEMBE...MORRISON KAMA KAWA 'ANAKULA BATA'...