Home Habari za michezo KUHUSU UKWELI WA FEI TOTO KULA UGALI NA SUKARI….MAMA YAKE AANIKA UKWELI...

KUHUSU UKWELI WA FEI TOTO KULA UGALI NA SUKARI….MAMA YAKE AANIKA UKWELI WOTE HADHARANI…

Tetesi za Usajili Yanga

Mama mzazi wa aliyekuwa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amnedai kuwa mwanaye huyo amenyanyasika akiwa ndani ya Klabu hiyo ndiyo maana akaamua kuomba haki yake.

“Fei amedharirika sana mpaka hapa ilipofikia sasa ndio maana nimeona sio wakati wa kuficha ni bora niweke hadharani. Naomba TFF huyu mtoto imtendee haki yake, Fei imefika wakati wakati akawa anakula ugali na sukari, leo ndiyo nasema sasa. Kwa kutetea haki yake lakini alikuwa anaficha.

“Feisal ni mchezaji wa taifa, leo amekaa kama mtu aliyeua wakati anadai haki yake. Ilifika wakati anakwenda kwenye mazoezi na bodaboda na pesa ya kumlipa hana lakini kwa vile anafahamiana naye anamkopa.

“Inafika wakati anakosa hata pesa ya matumizi ananipigia simu kuniomba na mimi ninamtegemea yeye mengine siwezi kuyasema. Alikuwa anajituma kwa sababu ya ndugu zake.

“Nataka TFF wasome shitaka la Fei walisome kwa Kiswahili ili kila mtu ajue aliyoyapitia. Fei sasa hivi hana furaha na Yanga bora aondoke tu, mtoto kateseka sana. Amepambana kwa njia za kawaida kuwaomba wamuongezee maslahi yake lakini wakaona hana thamani,” amesema Mama Fei.

Ikumbukwe kuwa, Fei aliandika barua kuomba kuondoka Yanga lakini klabu iligoma hivyo akaamua kuondoka klabuni hapo.

Kufuatia jambo hili, Yanga walifungua shauri TFF ambapo baada ya vikao vingi jana Kamati ya Hadhi na haki ya wachezaji ya TFF ilimuidhinisha Feisal Salum, kuwa mchezaji wa Yanga.

SOMA NA HII  BAADA YA ENZI ZA KAGERE KUISHA..SIMBA WAKOMAA NA MATIZI MAKALI KWA MUGALU..MWENYEWE AJIONGEZA..