Home Uncategorized MKWARA WA RUVU SHOOTING ACHA KABISA, WAPANIA KUSEPA NA UBINGWA

MKWARA WA RUVU SHOOTING ACHA KABISA, WAPANIA KUSEPA NA UBINGWA


 UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa malengo yao makubwa kwa msimu wa 2020/21 ni kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.


Kwa sasa bingwa mtetezi ni Simba ambaye alitwaa taji hilo mara tatu mfululizo na kwa sasa yupo nafasi ya ili na pointi 35 baada ya kucheza mechi 15.


Kinara ni Yanga ambaye amejikusanyia pointi 44 akiwa amecheza jumla ya mechi 18 na hajapoteza mchezo hata mmoja.


Mchezo wa Ruvu Shooting uliopita ulikuwa ni dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mabatini na ilisepa na ushindi wa mabao 2-0.


 Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ametamba kuwa msimu huu malengo yao ni kutwaa ubingwa au kumaliza kwenye nafasi tatu za juu.


“Malengo yetu ni kutwaa ubingwa au kumaliza nafasi za juu na raundi hii tunakuja na mfumo unaitwa PTK yani Papasa Tingisha, Kung’uta.


“Ukianzia kwa wachezaji, benchi la ufundi kote wapo imara na kila mmoja anafanya kazi yake kwa kujituma na kutimiza majukumu yake ipasavyo,” amesema.
 
Ruvu chini ya Kocha Mkuu, Charles Mkwasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu bara na alama 28 baada ya kushuka uwanjani mara 17.

Kwa timu zilizo ndani ya tatu bora, imepoteza pointi mbele ya Yanga kwa kufungwa mabao 2-1 Uwanja wa Mkapa.

Simba iliyo nafasi ya pili ilinyooshwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru huku Azam FC ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 Uwanja wa Azam Complex.
SOMA NA HII  NAMUNGO FC: BADO TUNA KAZI KIMATAIFA