Home Uncategorized SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MKUDE KUFUKUZWA SIMBA

SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA MKUDE KUFUKUZWA SIMBA


 OFISA Habari wa Klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kuwa kiungo mzawa Jonas Mkude hajafukuzwa ndani ya kikosi hicho bali suala lake lipo kwenye kamati ya nidhamu.


Desemba 28, taarifa rasmi kutoka Simba ilieleza kuwa kiungo huyo ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amesimamishwa ndani ya kikosi hicho kutokana na utovu wa nidhamu.


Tayari amekosa mechi mbili ambapo ya kwanza ilikuwa ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Majimaji na ule wa pili wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ihefu FC zote zilichezwa Uwanja wa Mkapa.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam,leo Januari 4 Manara amesema suala la mchezaji Jonas Mkude bado lipo kwenye kamati ya nidhamu ya Simba.


“Kuhusu Jonas Mkude ijulikane tu kuwa mpaka sasa ni sehemu ya Simba hajafukuzwa kazi, amepitia changamoto kama mfanyakazi mwingine kokote.


“Mkude ni mchezaji wa Simba. Jambo lake lipo kamati ya maadili. Mkude hajafukuzwa Simba. Bila shaka yoyote baada ya kamati atarejea klabuni. Huyu ndiye mchezaji mwandamizi ndani ya Simba kwa miaka 10.” amesema.

 

Simba ina kibarua cha kumenyana na FC Platinum Januari 6, Uwanja wa Mkapa ikiwa ni mchezo wa marudio baada ya ule wa kwanza kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Ili kutinga hatua ya makundi ina kazi ya kusaka ushindi wa mabao zaidi ya mawili na kulinda lango lao lisiguswe na wapinzani.

 

SOMA NA HII  ISHU YA KIONGOZI YANGA KUDAI KUIBIWA NA MASHABIKI WA COASTAL UNION IPO HIVI