Home Habari za michezo HIKI HAPA NDIO KILICHOMPONZA ROBERTINHO MBELE YA AL AHLY

HIKI HAPA NDIO KILICHOMPONZA ROBERTINHO MBELE YA AL AHLY

Habari za Simba

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid mwenyewe anajiita Wakanda Republic amesema kuwa kilichomgharimu Kocha wa Klabu ya Simba, Robertinho na kusababisha kuondolewa kwenye michuano ya AFL ni kufanya mabadiliko ya haraka baada ya kupata bao la kuongoza.

Simba jana iliondolewa katika michuano hiyo kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya kupata sare ya jumla ya mabao 3-3 dhidi ya Al Ahly (kwa maana ya bao 2-2 nyumbani na bao 1-1 ugenini).

“Robertinho aliwahi kujaribu kui-lock mechi, kwa sababu dakika ya 70 unamuingiza mchezaji eneo la ulinzi ambaye ni Kennedy Juma muda ambao timu yako ipo kwenye presha ya kushambuliwa.

“Obviously muda ule Robertinho alienda kui-lock mechi na ndiyo sababu ambayo ilikuja kumpa tabu baada ya Al Ahly kupata goli.

“Kwa sababu kama unamuingiza Kennedy Juma dakika ya 70 mwalimu aliamini ndani ya dakika 20 ambazo zimebaki ataenda kukaba typically akaweka timu kwenye block ya chini.

“Muda huo ndio ambapo Al Ahly wakaja Full Charge wote wakajazana kwenye eneo la Simba na mabeki wao wakasogea juu ili wapate goli,” amesema Wakanda Republic.

SOMA NA HII  MENEJA WA YANGA NAE AJA NA HILI KWENYE MECHI YA SIMBA NA YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here