Home Uncategorized AFC YAIPANIA PAMBA LEO

AFC YAIPANIA PAMBA LEO

UONGOZI wa timu ya Arusha umesema kuwa leo hawatafanya makosa mbele ya Pamba FC kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza.

AFC Arusha mchezo wake wa mwisho ilichapwa mabao 3-1 na Gwambina FCleo Febrari, Mosi itamenyana na Pamba ya Mwanza Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 Ofisa Habari wa AFC, Bahati Msilu amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani na watapambana kufanya vizuri leo.

“Ushindani ni mkubwa nasi tunaendelea kupambana ili kupata matokeo, makosa yaliyopita tunayafanyia kazi ili tushinde na kupata pointi tatu muhimu,” amesema Msilu.
SOMA NA HII  NYOTA HAWA WA YANGA WANARUDI NYUMBANI CHAMAZI LEO