Home Uncategorized MKENYA ANAYEKIPIGA NDANI YA SIMBA QUEENS ATAJA SABABU ZA KUCHEZA SOKA

MKENYA ANAYEKIPIGA NDANI YA SIMBA QUEENS ATAJA SABABU ZA KUCHEZA SOKA


 HUYU hapa Omita Bertha nyota anayekipiga ndani ya kikosi cha Simba Queens inayoshiriki Ligi ya Wanawake Tanzania wakiwa mabingwa watetezi wa taji hilo chini ya Kocha Mkuu, Mussa Mgossi

“Mimi nimezaliwa Kenya mkoa unaitwa Siaya. Nimelelewa na mama pekee na sikuwahi kupata nafasi ya kumjua baba yangu. Shule ya msingi nilisoma Awelo Primary School.


“Sekondari nikasoma Aluor Girls High School, nikafaulu vizuri na baadae nikaenda kusoma chuo cha Jaramogi Oginga Odinga University of Science and Technology. Nimesomea ualimu, Degree in English and Literature.

Ulianzeje kucheza soka?

“Kuhusu soka, nilipenda tangu nikiwa mdogo sana, wakati nipo shule kuna rafiki yangu alikuwa ananipeleka kwenye timu yao iliitwa Wadadia.

“Bahati, nilicheza vizuri wakasema wananichukua na kuanzia hiyo siku Mungu alinisaidia sana na nilikua nacheza kila mara nikipewa nafasi na kwenye mechi watu walikua wananiona na kuniamini.

“Baada ya hapo nikapita The Oserian Ladies, Kisumu All Starlets na ndipo Simba Queens, kwahiyo kwa ujumla nimecheza timu nne hadi sasa.

Uliwahi kuwa na ndoto kucheza Bongo?

“Sikuwahi kujua kua kuna siku nitawahi kuja kucheza ligi ya Tanzania, kwahiyo naweza kusema ni kama Mungu tu amependa nije huku.

“Mimi nilitaka nicheze mpira ‘Professionally’ kwanza hadi nifike mbali. Lakini ndoto yangu nyingine ilikuwa nisome niwe mwalimu na hapa ninapoingea na wewe nimesomea ualimu wa Sekondari.

Kuna timu ziliwahi kukufuata mbali na Simba?

“Huku Kenya kuliwa na timu nyingi sana ambazo zilikuwa zinanihitaji, lakini kwa Tanzania ilikuwa ni Simba na Baobab Queens.

Tofauti ya ligi ya Bongo na Kenya ipo wapi?

“Kuna tofauti kwasababu Kenya mechi nyingi ni ngumu sana, lakini kwa Tanzaniz naweza kusema ni Simba JKT, Yanga labda na Ruvuma. Halafu pia huku kuna kukamiana sana.

Mechi yako ya kwanza ndani ya Simba ilikuaje?

“Nilikua na furaha sana maana mashabiki walikuwa wengi wakitupa sapoti na hicho ndiyo kitu kitamu sana kwenye soka. Hiyo Simba Day jinsi watu walivyojaa uwanjani na pia jinsi ambavyo watu wanapenda soka ilinishangaza sana.

Matarajio yako ndani ya Bongo yapoje?

“Sidhani kama nimekuta tofauti kubwa sana maan nilijua wao ni mabingwa na kazi kubwa ilikua inatungnja msimu ukianza,” anamaliza

Kutoka Championi
SOMA NA HII  KIUNGO WA SIMBA ATIBUA DILI LA NYOTA WA RWANDA KUTUA YANGA