Home Habari za michezo WAKATI JAMBO LA CHAMA LIKIWA TETE….BENCHIKHA AMPIGA MKWARA MZITO PHIRI…

WAKATI JAMBO LA CHAMA LIKIWA TETE….BENCHIKHA AMPIGA MKWARA MZITO PHIRI…

Moses Phiri

Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha ametoa onyo kwa mastaa wa klabu hiyo, ambao wamepewa nafasi nyingi kupitia michuano ya Mapinduzi ambao walikuwa hawapati nafasi ya kucheza kuitumia vyema ili kumshawishi kuweza kuingia katika kikosi chake akiwemo nyota Moses Phiri.

Phiri tangu kuanza kwa msimu huu amekuwa hapati nafasi ya kutosha huku kwenye michuano ya Mapinduzi inayoendelea kutimua vumbi visiwani Zanzibar amekuwa akipewa nafasi mara kwa mara na amefanikiwa kufunga bao moja.

Kocha Benchikha amesema: “Kwa wale wachezaji wote ambao walikuwa hawapati nafasi ya kucheza mara kwa mara, tumejaribu kuwapa nafasi ya kutosha ili waweze kuonyesha mabadiliko na kulishawishi benchi la ufundi.

“Kwa hali nyingine, hii ni kawaida lakini kwa wachezaji wanatakiwa kupambana ili kuleta ushindani wa namba na hapo itakuwa ni faida ya timu kwa kuwa maendeleo yatakuwa yanapatikana kupitia wachezaji kujituma, ili walinde nafasi zao.

Gamondi aandaa mfumo mpya Young Africans
“Sisi kama Simba SC na ukubwa wa hii timu, hatutaki kuona mchezaji anajihajikishia namba kwani tunataka ushindani na ndio maana wamepewa nafasi kupitia hii michuano ili waweze kulishawishi benchi la ufundi” amesema kocha huyo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHO..MO DEWJI AUNGURUMA SIMBA...ADAI LAZIMA WAARABU WATISHWE...