Home epl MANCHESTER CITY YAPELEKEWA MBELE SIKU YA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU ENGLAND

MANCHESTER CITY YAPELEKEWA MBELE SIKU YA KUTWAA TAJI LA LIGI KUU ENGLAND

 

KUPOTEZA kwa Manchester City mbele ya Chelsea kumewapunguzia kasi ya kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England kwa kuwa waliacha pointi tatu mazima. 

Kwa kuyeyusha pointi hizo kwa sasa ni sawa na kusema kwamba Chelsea imewapeleka mbele siku ya City kutwaa taji hilo kwa kuwa wanapewa nafasi kubwa ya kuweza kulichukua mikononi mwa Liverpool iliyo nafasi ya 6 na pointi 57.

Raheem Sterling alianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 44 ila Sergio Aguero alikosa penalti baada ya kutaka kufunga kwa mtindo wa Panenka.

Ni Hakim Ziyech dakika ya 63 na Marcos Alonso dakika ya 90+3 alipachika bao la ushindi na kufanya iwe ni wiki njema kwa Kocha Mkuu, Thomas Tuchel.

Pep Guardiola wa Manchester City bado anaweza kutwaa taji hilo wiki hii ikiwa Manchester United watakwama kushinda mbele ya Aston Villa.

Ni miaka nane ilikuwa imepita kwa Arguero baada ya kufunga bao muhimu lililowafanya City kuwa Mabingwa ila jana Panenka yake ilikwama kuipa taji City mbele ya Chelsea. 

Kwenye msimamo City ipo nafasi ya kwanza na pointi 80 Chelsea ipo nafasi ya tatu na pointi 64 zote zimecheza mechi 35.


SOMA NA HII  BECKHAM NA INTER YAKE WAMKOMALIA MESSI...WATAKA JAMBO LIWE HARAKA...