Home news NABI AMRUDISHA DIARA…MAYELE, NTIBAZONKIZA KAMA KAWA…’SURE BOY’ AENDELEA KUCHOMA MAHINDI..

NABI AMRUDISHA DIARA…MAYELE, NTIBAZONKIZA KAMA KAWA…’SURE BOY’ AENDELEA KUCHOMA MAHINDI..


KOCHA Nasreddine Nabi wa Yanga amemuanzisha kipa Djigui Diarra katika mchezo wa kombe la Azam Shirikisho hatua 16 bora dhidi ya Biashara United unaochezwa leo saa 1:00 usiku katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Diarra anarejea baada ya kumaliza majukumu ya timu yake ya Taifa Mali iliyokuwa inashiriki fainali za mataifa Afrika (Afcon).

Kipa huyo leo ana kazi ya ziada kuonyesha uwezo wake kwa sababu mwenzake Abuutwalib Mshery alionyesha kiwango kizuri kwenye mechi alizocheza.

Wakati Diarra akirejea kocha Nabi amemuanzisha winga, Farid Mussa kama beki wa kushoto katika mchezo huu.

Mchezaji huyo anacheza kama beki baada ya Yassin Mustapha, David Bryson na Kibwana Shomari kuwa majeruhi.

Farid kwenye eneo la ulinzi atakuwa anacheza na sambamba na Paul Godfrey ‘Boxer’, Bakari Mwamnyeto na Yanick Bangala.

Wachezaji wengine katika eneo la kiungo ni Zawadi Mauya, Khalid Aucho, Jesus Moloko na Saido Ntibanzokiza.

Eneo la ushambuliaji wameanza Feisal Salum na Fiston Mayele.

SOMA NA HII  BAADA YA TETESI ZA KUSEPA KWAKE KUZAGAA LEO....CEO WA YANGA KASEMA NENO HILI TU MOJA...