Home news PAMOJA NA KUSHINDWA KUFUNGA JUZI…PABLO AFUNGUKA HILI KUHUSU JOHN BOCCO…ADAI HAKUNA HAJA...

PAMOJA NA KUSHINDWA KUFUNGA JUZI…PABLO AFUNGUKA HILI KUHUSU JOHN BOCCO…ADAI HAKUNA HAJA YA…


LICHA ya Nahodha wa Simba, John Bocco kushindwa kufunga kwenye mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu, lakini Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema mshambuliaji huyo atawashangaza kwa kuwa ni mfungaji bora.

Simba ikiwa imecheza mechi 15 za ligi, imetupia mabao 16 na kinara ni Meddie Kagere mwenye mabao matano na pasi moja ya bao, huku Bocco akiwa bado hajatupia bao kwenye ligi msimu huu licha ya msimu uliopita kuwa mfungaji bora na mabao 16.

Akizungumza na gazeti la  Spoti Xtra, Pablo alisema kuwa hana hofu na uwezo wa Bocco, hivyo anaamini kwamba atawashangaza wengi kadiri siku zinavyokwenda.

“Ninaye hapa mfungaji bora wa viwango ambaye anacheza Simba (Bocco), anapitia katika kipindi cha mpito na ninajua kwamba anapenda kufunga na atafanya hivyo bila mashaka.

“Ikiwa una mfungaji bora, hakuna haja ya kuwa na mashaka kwa kuwa muda upo na kuna masuala mengine ambayo yanatokea kama uchovu na ushindani kuwa mkubwa, hilo tumeliona na tumelifanyia kazi,” alisema.

Bocco ambaye msimu huu amekuwa akikosolewa sana kutokana na kushindwa kufanya vizuri, juzi Jumapili alionekana shujaa katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas wa Kombe la Shirikisho Afrika ambapo kuingia kwake kulibadili mambo.

SOMA NA HII  SAA KADHAA KABLA YA SIMBA KUKIPIGA NA WAGANDA...MBRAZILI KUMBE ALISHAMALIZA KAZI KITAMBO TU...