Home news PAMOJA NA MASIFAA YOOTE ANAYOPEWA….MAYELE ATUMIA DAKIKA 1,161 KUFUNGA GOLI SABA TU…

PAMOJA NA MASIFAA YOOTE ANAYOPEWA….MAYELE ATUMIA DAKIKA 1,161 KUFUNGA GOLI SABA TU…


FISTON Mayele, mzee wa kutetema, dozi yake anayotoa kwa kuwatungua wapinzani wake ni mwendo wa mojamoja kwa kuwa hakuna timu ambayo ameifunga mabao zaidi ya moja.

Straika huyo mwenye mabao saba, alianza kuwatungua KMC na langoni alikuwa amekaa Faroukh Shikalo kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Majimaji, Songea.

Azam FC ilikuwa timu ya pili kufungwa kisha ikafuata Mbeya Kwanza na biashara iliendelea mpaka walipokutana na Biashara United. Dodoma Jiji walikutana na joto ya jiwe na hatua nyingine ikawa mbele ya Coastal Union ya Tanga na msumari wake wa saba aliwatungua Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu Complex.

Hata kwa upande wa pasi bado ni mwendo wa mojamoja kwa kuwa alitoa pasi yake ya kwanza mbele ya KMC bao likifungwa na Feisal Salum na ile ya pili alitoa mbele ya Polisi Tanzania ilikuwa mbele ya Polisi Tanzania na mtupiaji alikuwa ni Dickson Ambundo. Mayele raia wa DR Congo amecheza mechi 15 na kutumia dakika 1,161.

SOMA NA HII  KISA KUSHINDWA KUFUZU KOMBE LA DUNIA...KOCHA TAIFA STARS AELEKEZA LAWAMA ZOTE HUKU..