Home news YANGA vs KAGERA NI VITA YA KISASI LEO…NABI AFUNGUKA NAMNA ATAKAVYOJIPIMIA…BARAZA AWAVIZIA…

YANGA vs KAGERA NI VITA YA KISASI LEO…NABI AFUNGUKA NAMNA ATAKAVYOJIPIMIA…BARAZA AWAVIZIA…


LEO Uwanja wa Mkapa uliopo Temeke, Dar es Salaam, itakuwa ni vita ya kisasi kwa Yanga inayonolewa na Nasreddine Nabi dhidi ya Kagera Sugar inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara. 

Yanga ni vinara katika Ligi Kuu Bara, mchezo wa kwanza walishinda bao 0-1 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera na mtupiaji alikuwa ni Feisal Salum, ambaye leo ataukosa mchezo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Baraza raia Kenya, alisema wanatambua Yanga ni timu imara na haijapoteza mchezo msimu huu, hivyo wataingia kwa tahadhari katika kujilinda na kushambulia.

“Mchezo wetu na Yanga utakuwa mgumu, lakini timu itakayoweza kumiliki eneo la kati ina nafasi kubwa ya kushinda. Kucheza mechi 15 bila kufungwa hilo ni jambo kubwa,” alisema Baraza.

Nabi alisema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila amewaambia wachezaji wake wacheze kwa juhudi. “Nimewaambia wachezaji wacheze kwa kujituma, nitakosa huduma ya Dickson Job ambaye ana adhabu,

Chico Ushindi huyu alikuwa nje kwa muda kutokana na majeraha, hivyo anaweza kuanza ama kutokuanza kwa kuwa bado hajawa fiti, Yassin Mustapha yupo safi, Kibwana Shomari hatacheza pia,” alisema Nabi.

Nyota wa Kagera Sugar, Hamisi Kiiza, alisema akipata nafasi atafunga ama atatoa pasi ya bao, lakini hataki kupata kadi katika mchezo huo.

“Ikiwa nitapata nafasi nitafunga ama kutoa pasi ya bao, lakini sitaki kupata kadi ya njano ama nyekundu kwenye mchezo wetu,” alisema Kiza ambaye aliwafunga Simba walipocheza Kaitaba.

SOMA NA HII  KUMBE, JUMA MWAMBUSI BADO YUPO YANGA