Home Uncategorized YANGA YA GSM NOMAA.. YASHUSHA BEKI KISIKI KUTOKA RWANDA..!!

YANGA YA GSM NOMAA.. YASHUSHA BEKI KISIKI KUTOKA RWANDA..!!

BAADA ya kumalizana na Winga Mkongomani, Tuisila Kisinda Yanga wamenasa tena saini ya beki Mnyarwanda, Erick Rutanga ambaye amewaambia mashabiki wasubirie utamu wake Taifa.

Rutanga ameliambia Mwanaspoti kwamba ni kweli amesaini na sasa anakuja kikazi zaidi huku akiwaambia waandae straika wa kutupia tu kwenye nyavu kwani, majalo zake watazipenda.

Yanga imemsainisha mkataba wa miaka miwili Rutanga akitokea Police ya Rwanda na sasa ana subiri kujiunga tu na kikosi hicho cha kocha Mbelgiji Luc Eymael.

“Mimi kama unavyojua nacheza beki ya kushoto, nakuja kuhakikisha Yanga haisumbuliwi huko najua kukaba. Yanga waondoe shaka,” alisema Rutanga ambaye Mwanaspoti linajua alisaini Police mwezi uliopita lakini amenunua mkataba wake akasepa. Rutanga alisema kwamba ubora wake mwingine ni kupiga krosi kali za mabao.

“Zile krosi zangu nilizokuwa napiga Rayon na hata Police sasa zinahamia Yanga nasikia watasajili washambuliaji wazuri acha wawalete watafurahia kazi yangu.

“Hakuna kinachoshindikana katika kuwapa krosi washambuliaji nina uzoefu wa kutosha katika jukumu hilo, lakini pia hata inapotokea mipira ya adhabu najua sana kupiga.”

NIYONZIMA, SIBOMANA

Alisema safari yake ya kukubali mkataba wa miaka miwili utakaomfanya kulipwa kiasi cha dola 25,000 (sh 57.5 milioni), raia wenzake kiungo Haruna Niyonzima na winga Patrick Sibomana walihusika kumvuta klabuni hapo.

“Nilipofuatwa na Yanga hatua ya kwanza niliwatafuta Haruna (Niyonzima) na Patrick (Sibomana) walifurahia kusikia hivyo na wakaniambia nisaini haraka kwani, mambo yamebadilika ndani timu kuna wadhamini wengi, nikaona nisaini haraka walinitumia mkataba na nikasaini,” alisema

Kabla ya ujio wa Rutanga Yanga ilikuwa ikiyumba kutafuta mtu sahihi katika beki ya kushoto baada ya Adeyun Saleh kushindwa kutamba na Kocha kulazimika kumtumia na Japhary Mohamed.

SOMA NA HII  KICHAPO CHA MABAO 5-2 WALICHOPOKEA CITY GUARDIOLA ASEMA NI PRESHA