Home Uncategorized STARIKA YANGA AOMBA KUTUA MSIMBAZI

STARIKA YANGA AOMBA KUTUA MSIMBAZI

STRAIKA Mghana Michael Sarpong ambaye Kocha wa Yanga, Luc Eymael aliwaambia viongozi wamsainishe, muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa Msimbazi.

Eymael alikuwa amempendekeza straika huyo kwa anaielewa shughuli yake, lakini na dau lake likawashinda.

Sarpong amegoma kusaini mkataba mpya na Rayon Sports baada ya ule wa awali kuvunjwa kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, ameliambia Mwanaspoti kuwa; “Nasaini Simba.”

Mchezaji huyo aliyetupia mabao 16 msimu uliopita na kuwapa Kombe Rayon, alisema wapo hatua nzuri ya mazungumzo na Simba na anaweza kusaini.

“Kuna mazungumzo yanaendelea vizuri sana na nadhani dili linaweza kumalizika muda wowote, mkataba unashughulikiwa kati ya wakala wangu na Simba,” alisema Sarpong ambaye Eymael anamuelewa sana.

“Kuna vitu vidogo sana vimesalia kwenye makubaliano yetu na Simba,” alisisitiza Sarpong mwenye miaka 24 kwa mujibu wa hati yake ya kusafiria.

Sarpong, alijiunga na Rayon Septemba 2018 na akatamba kwa misimu miwili na amesisitiza kwamba, kama wakimalizana kila kitu na Simba basi atakuja kuonyesha makali yake Ligi Kuu Bara msimu ujao.

“Naamini nikisaini Simba nitafanya vizuri sana, nahitaji tu mazingira mazuri ya kufanya kazi, sikuwahi kushindwa kweye soka,” alitamba straika huyo ambaye kisa cha kuchaniwa mkataba na Rayon ni kuwajibu mbovu viongozi wake ambao walimshauri kupunguza mshahara wake kisa virusi vya corona.

SOMA NA HII  SAMATTA AINGIA ANGA ZA FULHAM