Home Uncategorized SABABU YA MBELGIJI KUMRUDISHA AJIBU SIMBA B, HIZI HAPA….

SABABU YA MBELGIJI KUMRUDISHA AJIBU SIMBA B, HIZI HAPA….


Kutokana na kutokuwa na uhakika wa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Simba, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Ibarahim Ajibu, pamoja na wenzake wasiokuwa na nafasi katika kikosi cha kwanza, Ijumaa ijayo wanatarajiwa kupelekwa Simba B.

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck amewaandalia wachezaji hao mechi ya kirafiki na Simba B ambayo watacheza kwa ajili ya kuongeza viwango vyao katika kipindi hiki ambacho michuano ya Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa.

Sven alisema kuwa mchezo huo ni moja ya mikakati yake ya kuhakikisha wachezaji wote ambao hawana nafasi katika kikosi chake cha kwanza wanautumia katika kuongeza uwezo wao.

“Licha ya ligi kusimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa, sisi tunaendelea kujifua kama kawaida.

“Tunafanya mazoezi ya nguvu ambayo yanalenga kabisa kuwaweka sawa wachezaji wote ili waweze kuwa fiti na zaidi ni wale ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza.

“Kwa hiyo, siku ya Ijumaa tutakuwa na mechi ya kirafiki na Simba B, wachezaji ambao watapambana na timu hiyo zaidi watakuwa ni wale ambao hawana nafasi katika kikosi cha kwanza,” alisema Sven.

SOURCE: CHAMPIONI
SOMA NA HII  HIZI HAPA LEO 18 UWANJANI KUSAKA POINTI TATU