Home Simba SC SIMBA YATAKA KUSEPA NA MAKOMBE YOTE BONGO

SIMBA YATAKA KUSEPA NA MAKOMBE YOTE BONGO


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wamejipanga kuchukua makombe yote ambayo wanashiriki msimu huu ndani ya ardhi ya Tanzania. 

Simba inashiriki Ligi Kuu Bara inaongoza ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 25 pia inashiriki Kombe la Azam Federation ikiwa imetinga hatua ya robo fainali.

Baada ya droo kupangwa jana Mei 11 itakutana na Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu,  Mbwana Makata na itakuwa ni mara ya tatu kukutana nayo uwanjani kwa kuwa katika mechi mbili za ligi, Simba ilishinda mechi zote nje ndani.

Inatarajiwa kukutana na Dodoma Jiji kati ya Mei 25-27, Uwanja wa Mkapa. Katika mataji hayo yote mabingwa watetezi ni Simba wenyewe.

Gomes amesema:”Katika kila mashindano ambayo tutashiriki tunahitaji kubeba ushindi na haitakuwa rahisi ni muhimu kwa kila mchezaji kupambana, “.

Kwa sasa Simba ipo nchini Afrika Kusini ikiwa katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya Kwanza dhidi ya Kaizer Chiefs,  Mei 15.


SOMA NA HII  SHAFFIH DAUDA:- MADHAIFU YA SIMBA YAPO KWA INONGA...CHE MALONE ANAZIBA MAKOSA YAKE...