Home Uncategorized RASMI…MSAUZI AMUONDOA TSHISHIMBI YANGA..!!

RASMI…MSAUZI AMUONDOA TSHISHIMBI YANGA..!!

NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi hatacheza mechi ya  keshokutwa dhidi ya Namungo.

Tshishimbi alikuwa anafikiri angeweza kucheza mchezo huo na tayari alishajiandaa lakini mmoja wa watalaam wa kigeni katika benchi lao amemzuia akimwambia atulie bado kidogo.

Taarifa ya kitabibu iliyotolewa na daktari mkongwe wa timu hiyo, Shecky Mngazija ni kwamba nahodha huyo amezuiwa na mtaalam wa tiba ya viungo Fareed Caseem.

“Tshishimbi hataweza kuwa tayari kwa mchezo huo. Kuna maelekezo mapya yametolewa na daktari mwenzangu wa tiba ya viungo kwahiyo hatacheza,” alisema Mngazija.

Mngazija aliongeza kuwa Caseem, raia wa Afrika Kusini anataka kuona anapona vizuri kabisa.

“Anachotaka (Caseem) ni kuona Tshishimbi anapona kabisa ili akirudi awe sawa ndio sababu kubwa ya uamuzi huu na tayari tumeshawapa taarifa makocha kwa hatua nyingine za kikazi,” alisema Dk Mngazija.

Baada ya taarifa hizo gazeti la Mwanaspoti ilimtafuta nahodha huyo ambaye alionyesha kuumizwa na akisema amelazimika kuwaelewa madaktari wake.

“Nilikuwa nadhani ningeweza kucheza, lakini nilipokutana na madaktari wameniambia hivyo kwamba nitakuwa nje kwa muda zaidi,” alisema Tshishimbi.

SOMA NA HII  WINGA AS VITA: NIMEFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA