Home Habari za michezo WAKATI NABI AKIIKIMBIA YANGA…MORRISON ‘AMFANYIA UDALALI WA KAZI MPYA’ AFRIKA KUSINI…

WAKATI NABI AKIIKIMBIA YANGA…MORRISON ‘AMFANYIA UDALALI WA KAZI MPYA’ AFRIKA KUSINI…

Habari za Yanga SC

STRAIKA wa zamani wa Orlando Pirates, Bernard Morrison amewaambia Kaizer Chiefs kwanini Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi ni chaguo sahihi kwao kwa sasa.

Morrison ambaye ni kipenzi cha mashabiki wa Yanga, amewaambia Kaizer kwamba miaka miwili ya Nasreddine Nabi Jangwani amejifunza mengi na ameiva kuchukua nafasi ya Arthur Zwane anayetajwa kulipwa Sh100milioni kwa mwezi.

Morrison alinukuliwa na Gazeti la FARPost la Afrika Kusini jana kwamba; “Anajua kwamba kwenye hizi klabu kubwa,ukipoteza moja na sare moja umeondoka. Kwahiyo anajua presha iliyopo.”

“Amekuwa hapa Yanga kwa karibu miaka miwili, nadhani kwenda kwenye klabu kubwa kama za Afrika Kusini anajua jinsi ya kudili na presha. Anajua kwamba lazima apate matokeo mazuri, kama hatayapata watamtimua.

“Kwahiyo lazima awe tayari kwa hali yoyote,”alisema Morrison ambaye anahusishwa na klabu ya Singida United msimu ujao.

Habari za uhakika ni kwamba Nabi jana alikuwa kwenye mazungumzo na Kaizer na amewaambia mambo kadhaa anayotaka ikiwemo timu yake ya ufundi na yeye inaelezwa atalipwa donge nono la Sh100milioni anazolipwa Kocha wa sasa ambaye wanataka kumtoa baada ya kushindwa kutimiza malengo.

Nabi amewaambia anataka kwenda na Kocha Msaidizi, Kocha wa Makipa pamoja na mtu wa video na inaripotiwa siku yoyote wiki hii atatua Sauzi kumaliza dili.

Tayari jana Yanga walitangaza kuachana na Nabi ambaye mkataba wake uliisha mwishoni mwa msimu huu kwenye mechi ya Fainali ya kombe la Azam Sports Cup Federation dhidi ya Azam FC ambapo Yanga walishinda.

SOMA NA HII  MUDATHIR AVUNJA UKIMYA AZAM...AFUNGUKA KINACHOWAKWAMISHA..WACHEZAJI NA KOCHA WATAJWA..