Home Habari za michezo RASMI….YANGA WASALIMU AMRI KWA ISHU YA KUMPIGA BEI MAYELE…BEI YAKE YATAJWA…

RASMI….YANGA WASALIMU AMRI KWA ISHU YA KUMPIGA BEI MAYELE…BEI YAKE YATAJWA…

Habari za Yanga

BAADA ya kutetea taji lao la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), mabosi wa Yanga wamesema katika uongozi wao wapo tayari kumuuza mchezaji yeyote ambaye watapokea ofa nzuri.

Yanga ilitetea taji hilo kwa kuifunga Azam FC bao 1-0, fainali iliyochezwa Uwanja wa mkwakwani, jijini Tanga.

Hivi karibu Yanga wamemuuza kiungo wao Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyeenda Azam FC na kuna tetesi mshambuliaji wao bora Fiston Mayele huenda asiwe miongoni mwa mastaa wa timu hiyo msimu ujao. Fei ameuzwa kwa zaidi ya Sh200 milioni.

Akizungumza mara baada ya fainali za kombe hilo kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Seif Gulamali alisema kama kuna timu inamhitaji Mayele na ikitoa pesa nzuri basi hawana budi kumuuza.

“Hatuna sababu za kuzuia kumuuza mchezaji kama timu inayomtaka itatoa pesa nzuri, Yanga ni timu yenye wachezaji wazuri na wapo kwenye soko kwasasa na ndio maana tumepata mafanikio kwenye mashindano yote tuliyoshiriki msimu huu,” alisema Gulamali.

Rais wa klabu hiyo, Injinia Hersi Said alisema mipango yao ya msimu ujao ni kuboresha kikosi chao zaidi.

“Kwa sasa tulikuwa tunamalizia michezo yetu na kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa kwa kutetea makombe yetu na tumeweza huku tukifika fainali za Kombe la Shirikisho Afrika, ni mipango ambayo tulijiweke tangu miaka mitatu nyuma, hivyo nafanikio haya hayajaja kirahisi.

“Kuhusu usajili wa msimu ujao ni jambo ambalo lipo mbele yetu, ikiwemo kuongeza mikataba wachezaji ambao imemalizika na tunahitaji kuendelea nao,” alisema Hersi.

SOMA NA HII  TANZANIA U-20 WAANZA SAFARI YA MATUMAINI KUFUZU AFCON....