Home Habari za michezo EBWANA EHEE..ISHU YA BAJANA KUMBE BADO MBICHI ….SIMBA NA AZAM USO KWA...

EBWANA EHEE..ISHU YA BAJANA KUMBE BADO MBICHI ….SIMBA NA AZAM USO KWA USO…

Tetesi za Usajili Simba

Kiungo wa Azam FC, Sospeter Bajana ambaye anatajwa kuwaniwa na Simba SC amesema kwamba yupo kwenye mazungumzo na timu zote mbili na anachoangalia ni maslahi zaidi.

Bajana amesema bado hajafikia maamuzi ya wapi atacheza msimu ujao, na ni kweli kwamba klabu zote mbili zipo kwenye mazungumzo nae na anachoangalia zaidi ni maslahi.

“Sasa ni mapema kusema msimu ujao nitacheza wapi, kwa sababu mkataba wangu kwa sasa upo ukiongoni, nafanya mazungumzo na Azam FC kwa mkataba mpya, lakini Simba SC wameonesha nia, naangalia maslahi zaidi kwa sababu nina familia ambayo inanitegemea,” amesema Bajana.

Hata hivyo, uongozi wa matajiri Azam umewaka wazi kuwa utahakikisha wanafanikiwa kumbakiza mchezaji huyo kwa kumuwekea dau nono.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’, amesema wanashukuru Mungu kumaliza Ligi Kuu salama bila ya majeruhi yoyote makubwa na kuhakikisha wamepata nafasi ya kufuzu kucheza kombe la Shirikisho na sasa wanahitaji kuboresha kikosi chao.

Katika hilo, Popat amesema kuwa kwa sasa wanalazimika kuwabakiza baadhi ya wachezaji wao ambao mikataba yao ipo ukingoni akiwemo Bajana.

“Msimu ujao tunaenda kucheza kimataifa, tumeanza usajili wa nyota wa ndani kwa kumchukuwa Feisal Salum ‘Fei Toto’, tutasajili kulingana na mahitaji ya kikosi chetu na kuhusu Bajana haendi popote kwani tutakutana naye na kuzungumza nae kuhusu kumuongezea mkataba mwingine,” amesema Mtendaji huyo

Amesema wamedhamiria kuboresha kikosi chao na kuhakikisha wanafanya usajili wa wachezaji bora na kuwaongeza mikataba nyota wale wako kwenye mipango ya timu yao kwa msimu ujao.

SOMA NA HII  SIMBA YAFUNGUKIA SUALA LA ZAHERA KUWA KWENYE BENCHI LA UFUNDI