Home Habari za michezo BAADA YA KUUWASHA MOTO MORROCO…JINA LA OPAH LATUA RASMI CAF…HISTORIA YAWEKWA…

BAADA YA KUUWASHA MOTO MORROCO…JINA LA OPAH LATUA RASMI CAF…HISTORIA YAWEKWA…

Nahodha na Mshambulaiji wa Simba Queens Opah Clement, ametajwa kwenye kikosi bora cha Afrika mwaka 2022 kilichotangazwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.

Opah ametajwa kwenye kikosi hicho, baada ya kumalizika kwa Michuano hiyo nchini Morocco na wenyeji ASFAR Rabat kutwaa ubingwa wakiichapa Mamelodi Sundows Ladies ya Afrika Kusini 4-0.

Mshambuliaji huyo aliifungia Simba SC mabao mawili kwenye Michuano hiyo, akifunga dhidi ya Determine Girls FC ya Liberia, kisha akafanya hivyo kwenye mpambano wa mwisho Hatua ya Makundi dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

Hata hivyo Opah alionekana kuwa Mshambuliaji anayechungwa sana kwenye michezo yote iliyoihusisha Simba Queens, iliyomaliza katika nafasi ya nne, baada ya kupoteza mbele ya Bayelsa Queens ya Nigeria.

Tayari Simba Queens imesharejea nchini ikitokea Morocco, huku ikitarajia kuanza maandalizi ya Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu 2022/23.

SOMA NA HII  TRY AGAIN: SIMBA TUTASAJILI 'VIFAA' KUTOKA ARGENTINA NA URUGUAY