Home Habari za michezo PAMOJA NA KUWAFUNGIA MAGOLI 5, CHAMA LA MSUVA HUKO UARABUNI TIA MAJI...

PAMOJA NA KUWAFUNGIA MAGOLI 5, CHAMA LA MSUVA HUKO UARABUNI TIA MAJI TIA MAJI AISEE…

Saimon Msuva

LICHA ya kwamba chama lake, Al-Qadsiah FC halijauanza vizuri msimu huu wa Ligi Daraja la Kwanza Saudi Arabia, Mtanzania, Simon Msuva anaamini wanaweza kumaliza kwa kishindo huku wakipanda daraja.

Kabla ya mchezo wa juzi, Jumatatu ambao Al-Qadsiah FC ilikuwa nyumbani katika Uwanja wao wa Prince Saud bin Jalawi, walikuwa wakishika nafasi ya 13 kwenye msimamo wenye timu 18 wakiwa na pointi 12 kwenye michezo 11 waliyocheza.

Al-Qadsiah FC anayoichezea Msuva imeshinda michezo mitatu, ikitoka sare michezo mitatu, wamepoteza mara tano.

Akizungumzia mwenendo wao kwenye ligi, Msuva alisema; “Bado kama timu tunaamini kuwa tunaweza kubadilisha mambo, kila kitu kipo ndani ya uwezo wetu, tuna timu nzuri sema ni vile kuwa wachezaji wengi ni wapya hivyo inahitaji muda kuzoeana, hiyo haiwezi kuwa sababu ya kujitetea,” alisema.

Pamoja na ugeni wake kwenye ligi hiyo, Msuva ni miongoni mwa washambuliaji ambao wanapigania kiatu cha ufungaji bora akiwa na mabao matano, vinara ni Mbengue A. wa Al Arabi (11), akifuatiwa na Queiroz Bezerra wa Al Orubah akiwa na mabao tisa.

Msuva alijiunga na timu hiyo, Julai 24 mwaka huu baada ya kushinda kesi yake ya madai dhidi ya waajiri wake wa zamani Wydad Casablanca ambao waliagizwa na FIFA kumlipa zaidi ya dola za kimarekani 700,000 ( zaidi ya Sh 1.6 bilioni).

Nyota huyo ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne aliusitisha mkataba wake Disemba 2021.

SOMA NA HII  A-Z GUEDE ALIVYOJIBU MASWALI MAGUMU LEO....YANGA WAKINOA PANGA KWA DABI YA KARIAKOO...