Home Simba SC KOCHA MPYA SIMBA APANGA KUISHUSHA YANGA KILELENI MAPEMA

KOCHA MPYA SIMBA APANGA KUISHUSHA YANGA KILELENI MAPEMA


Kocha mpya wa Simba, Didier Gomes amesema kiu yake kubwa ni kutaka miamba hiyo kuizidi Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Pamoja na kutaka kuongoza ligi, Gomes raia wa Ufaransa alisema ushiriki wao katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni kitu muhimu na atahakikisha wanakuwa bora.

Akizungumza kabla ya kusaini mkataba mpya na mabingwa hao wa soka nchini, Gomes aliyechukua mikoba ya Sven Vandebroeck alisema anaijua Simba tangu akiwa katika klabu aliyotoka na anataka kuipa mafanikio zaidi.

“Huwezi kucheza Ligi ya Mabingwa bila kufanya vizuri katika ligi ya ndani, kwahiyo nataka kuhakikisha tunashinda mechi za ligi, Simba ni klabu ambayo inataka kila msimu kuwa katika mashindano makubwa ya Afrika.

“Nafahamu tunatakiwa kufanya vizuri pia katika mechi za hatua ya makundi. Niliiangalia timu hii wakati inawaondoa Platinum, ilinivutia sana na ndiyo maana nipo hapa, alisema kocha huyo wa zamani wa El Mereikh ya Sudan.

Amewasili nchini juzi, ikiwa ni muda mfupi tangu alipoacha kazi katika klabu hiyo ya Sudan na kusaini mkataba wa miaka miwili kuinoa mimba ya Msimbazi.

Gomes analijua soka la Afrika, kwani aliwahi kufundisha Horoya AC kuanzia Machi 20 hadi Novemba 2019, alipotimuliwa.

Aliwahi pia kuwa kocha wa Ismaily kuanzia Januari 8 hadi Agosti, 2020. Alisaini mkataba wa kuinoa Al Mereikh Novemba 14 202 hadi alipotangaza kuachana na timu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibukia Simba.

Huyo anakuwa kocha wa pili kutangazwa na Simba ndani ya wiki moja, baada ya Milton Nienov, aliyeletwa kama kocha wa makipa.

SOMA NA HII  ERNASTO NYONI APANGA KUGAWA TIKETI ZA BURE MCHEZO WA KESHO