Home Habari za michezo KOMBE LA DUNIA KUCHEZWA NDANI YA NCHI TATU….FIFA WAANIKA MIJI ‘KIVUMBI KITAKAPOTIFULIWA…’

KOMBE LA DUNIA KUCHEZWA NDANI YA NCHI TATU….FIFA WAANIKA MIJI ‘KIVUMBI KITAKAPOTIFULIWA…’


FIFA imetangaza Miji 16 ambako mechi za Kombe la Dunia 2026 zitachezwa.

Tangazo hili muhimu katika dunia ya soka limefanyika jijini New York likiongozwa na Rais wa FIFA Gianni Infantino.

Mashindano hayo yatafanyika katika nchi tatu Marekani,Canada na Mexico.

Mechi zitachezwa katika maeneo 11 ndani ya Marekani : Atlanta, Boston, Dallas, Houston, Kansas City, Los Angeles, Miami, New York /New Jersey, Philadelphia, San Francisco na Seattle.

Nchini Canada mechi zitachezwa katika miji ya Toronto na Vancouver, wakati nchini Mexico mechi zitachezwa Guadalajara, Mexico City na Monterrey.

Kombe la Dunia 2026 litakuwa la kwanza kuhusisha timu 48 zikiwa zimeongezeka timu 16 ukilinganisha na Kombe la Dunia la mwaka huu. Kombe hilo pia litakuwa la kwanza kufanyika katika nchi tatu.

SOMA NA HII  UMAKINI ANAO UTAKA BENCHIKHA UNAAMBIWA KAMA JESHINI