Home news TAARIFA MBAYA; WACHEZAJI WA POLISI TANZANIA 16 WAMEUMIA, ORODHA HII HAPA

TAARIFA MBAYA; WACHEZAJI WA POLISI TANZANIA 16 WAMEUMIA, ORODHA HII HAPA


 TAARIFA ambayo ni mbaya kwa ulimwengu wa michezo leo, Julai 9 ni kuhusu ajali waliyopata wachezaji wa timu ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassan Juma imeeleza namna hii:Leo majira ya saa 11:00 asubuhi timu ya Polisi Tanzania imepata ajali wakati ikitoka mazoezini kwenye uwanja wa TPC uliopo kwenye Kiwanda cha sukari TPC Moshi na kupelekea majeruhi kwa wachezaji 16 ambao ni
1. Gerald Mdamu – amevunjika miguu yote miwili
2. Abdullazizi Makame
3. Pius Buswita
4. Daruweshi Saliboko
5. Deusdedity Cosmas
6. Salum Ally
7. Abdulmaliq Adam
8. Idd Mobby
9. Marcel Kaheza
10. Shabani Stambuli
11. Yahaya Mbegu
12. Datusi Peter
13. Mohammed Bakari
14. Mohammed Yusuph
15. Kassim Haruna
16. Christopher John
17. George Mketo – dereva
18. Vicente Ngonyani – dereva

Wachezaji wote hawa wapo KCMC wakiendelea na uchunguzi wa daktari, chanzo cha ajali kinachunguzwa.

Mungu awalinde na kuwapa afya wachezaji wote, pia salamu kutoka timu mbalimbali zimekuwa zikitumwa ikiwa ni pamoja na Simba, Yanga, Azam FC, Tanzania Prisons.

SOMA NA HII  JINA LA INONGA BAKA LAINGIA KWENYE REKODI HIZI ZA CAF.....AFCON IKIZIDI KUMPAISHA JUU...