Home news POLISI TANZANIA WAPATA AJALI WAKITOKA MAZOEZINI

POLISI TANZANIA WAPATA AJALI WAKITOKA MAZOEZINI


 TIMU ya Polisi Tanzania, leo Julai 9 imepata ajali wakati ikitoka kwenye mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zinatarajiwa kuendelea Julai 14.

Taarifa rasmi iliyotolewa na Polisi Tanzania, kupitia akaunti rasmi ya Instagram ya Polisi Tanzania imeeleza namna hii:-Timu yetu imepata ajali wakati ikitoka mazoezini leo. Baadhi ya wachezaji wameumia.

Tunaomba mashabiki wetu na wapenda michezo waendelee kuwa na subira na taarifa rasmi itakujia hivi punde.


Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa kwa sasa wanashughulikia afya za wachezaji pamoja na wale ambao wameumia na taarifa rasmi zitatolewa.


SOMA NA HII  VIGOGO SIMBA NA YANGA WAJITOSA KUWANIA UBOSI WA BODI YA LIGI...