Home Habari za michezo BAADA YA GUEDE KUANZA KUTUPIA YANGA…AZIZ KI AFICHUA KILICHOKUWA KINAMTIA UGUMU…

BAADA YA GUEDE KUANZA KUTUPIA YANGA…AZIZ KI AFICHUA KILICHOKUWA KINAMTIA UGUMU…

Habari za Yanga leo

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI, amesema moto alioanza nao Joseph Guede bado kabisa kwani anamjua ni mchezaji hatari linapokuja suala ya kucheka na nyavu, sema alikuwa akijitafuta tangu atue Jangwani.

Aziz KI alisema Guede aliyefunga mabao matatu katika mechi mbili zilizopita, mawili katika Kombe la ASFC na lile muhimu zaidi lililoipeleka Yanga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ni mchezaji hatari na wale waliokuwa wakimchukulia poa, basi wajiandae kupata aibu wakati huu gari lake likiwa limeshaanza kuwaka.

Guede alifunga bao la nne wakati Yanga ikiizamisha CR Belouizdad kwa mabao 4-0, pasi yake ikitokea kwa Aziz KI ambaye alisema anamfahamu nyota huyo na kwamba moto wake bado haujawaka kisawasawa ila utawachoma wengi.

 Aziz alisema mabao ambayo ameanza kufunga Guede ni mwanzo tu kwani anamfahamu vilivyo uimara wake kwenye eneo la kucheka na nyavu.

Alisema uwezo atakaouonyesha utaendelea kuwashangaza kwani anamtambua mshambuliaji huyo vizuri. “Wakati akiwa FAR Rabat alikuwa akija Ivory Coast kwaajili mapumziko na walikuwa wakifanya mazoezi na niliwahi pia kumfuatilia kwa ufupi.

“Sina wasiwasi, atafunga sana ila alihitaji muda wa kuzoea mazingira na namna ya uchezaji lakini pia watu wasisahau kuwa alikuwa nje kwa kipindi kidogo. Mchezaji yeyote uwezo wake upo katika kucheza mechi kubwa zenye ushindani ndio maana alipokuja alikuwa na wakati mgumu wa kujitafuta kwanza ila kwa nafasi hizi anazopewa sasa mashabiki watamsahau,” alisema Aziz.

Nyota huyo Mghana ni miongoni mwa wachezaji 24 waliopo Cairo, Misri na kikosi cha Yanga kinachojiandaa na mechi ya kufungia makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly itakayopigwa kesho kuanzia saa 1:00 usiku, kila timu ikisaka heshima ya kumaliza kinara wa Kundi D kwani zote zimeshafuzu.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA YANGA WANAMZENGEA ZENGEA SANA...KIYOVU WATAKA MIL400 KUMUUZA BIGIRIMANA...